FURSA NA VITABU VYA BIASHARA
Wednesday, September 19, 2018
Thursday, August 24, 2017
Wednesday, August 23, 2017
UTUNZAJI WA KUKU NA MAGONJWA
Tunafahamu kwamba magonjwa ndio chanzo kikubwa cha kukatisha
ndoto za mfugaji kutokana na ughali wa bei za dawa au vifo vinavyosababishwa na
magonjwa hayo. Lakini upo uwezekano wa kuyaepuka hayo ikiwa tutazingatia
yafuatayo kwa uangalifu mkubwa:-
- Chanja kuku dhidi ya magonjwa mbalimbali yasiyotibika
kama vile mdondo, gumboro na ndui.
- Usifuge kuku na ndege wengine kama vile bata, kanga au
kwale katika banda moja. Pia usichannganye kuku wa asili na wa kisasa
katika banda moja, yaan kwa mfano usichanganye kuku wa nyama(broilers) na
kuku wa asili.
- Usirudishe nyumbani kuku waliopelekwa sokoni wakakosa
soko kwani wanaweza kuleta magonjwa.
- Ondoa kuku wote wenye dalili za ugonjwa na uwatibu kwa
dawa husika, na waliokufa wazike au wachome moto.
- Watenge kuku wageni kwa takribani wiki mbili kabla ya
kuwachanganya na wa zamani.
- Usafi wa banda, vyombo vya maji na kulishia, na
muhudumu ni vya kuzingatia pia.
- Zuia watu wasiohusika, au ndege kuingia au kukaribia
banda.
- Kuwepo mavazi na viatu maalum vya kuingilia bandani.
- Mlangoni kuwekwe dawa ya kuulia vijidudu kwa ajili ya
kukanyaga kabla ya kuingia bandani.
- Banda lipumzishwe wiki mbili kabla ya kuingiza kuku
wapya.
- Wape kuku chakula bora na maji safi na salaama. Maji
safi na salaama ni yale ambayo hata wewe mfugaji unaweza kuyanywa.
PATA KITABU HAPA |
Monday, January 16, 2017
NUNUA VIFAA MUHIMU SANA VYA UFUGAJI WA KUKU
Tunauza mashine za kutotolesha,cage za kufugia kuku,mashine za kutengeneza chakula cha kuku na Samaki,taa za joto kwa akili ya vifaranga,vifaa vya kupimia joto,mashine za kunyonyoa kuku kwa bei nafuu zaidi sana n.k
AFI GREEN EQUIPMENT CO LTD
Tunapatikana Dar es salaam,Mikocheni Victoria.Tupigie kwenye
namba 0624 181 003 au 0757 117 699.
Tunatuma mizigo nchi nzima na tunawafikia Wateja nchi nzima kwa uaminifu na uadilifu
Pia mawasiliano zaidi na ushauri zaidi:
0767 574 013
Wednesday, November 16, 2016
UANDAAJI WA CHAKULA CHA KUKU
RLDC na Uboreshaji wa Maisha Vijijini
Shirika la Rural Livelihood Development Company (RLDC ni moja ya mafanikio
ya ushirikaiano kati ya Tanzania na Uswisi kwenye mchakato wa kupambana na
umaskini na kuboresha maisha ya jamii za vijijini. Hii ni taasisi isiyo ya kibiashara
ili yoanzishwa mwaka 2005 na mashirika ya Intercooperation na Swisscontact,
lengo kuu likiwa kutekeleza Programu ya kuendeleza maisha ya jamii za vijijini
(RLDP). Programu hii inasha bihiana na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupambana
na Umaskini (MKUKUTA). Dhamira kuu ya RLDC ni Kuendeleza/kuboresha mifu
mo ya masoko ili kuwawezesha wazalishaji wa vijijini kutumia
fursa zilipo kuboresha maisha yao.
Kwa sasa, RLDC inatelekeleza awamu ya pili ya mpango wake (2008-2011)
na inaweka msukumo zaidi kwenye uendelezaji wa mifumo ya masoko. RLDC
inafanya kazi katika mikoa sita ya Kanda ya kati-Dodoma, Singida, Morogoro,
Shinyanga, Tabora, na Manyara. Jamii nyingi maskini zinaishi katika ukanda huu
wenye sehemu kubwa yenye hali ya mvua chache na nusu jangwa inayostawisha
shughuli chache za kiuchumi.
Hata hivyo kuna fursa nyingi sana zinazoweza kutoa ajira na kuboresha ya
jamii zake. RLDC inafadhiliwa na Serikali ya Uswisi kupitia shirika la Uswisi la
maendeleo (SDC).
Kwa sasa RLDC inawezesha sekta za pamba, alizeti, maziwa, ufugaji wa kuku wa
kienyeji, mpunga na habari kupitia vipindi vya redio kwa ajili ya wazalishaji wa
vijijini.
“RLDC inaboresha mifumo ya masoko ili kuwezesha wazalishaji wa
vijijini kuinua maisha yao”
Saturday, August 13, 2016
Subscribe to:
Posts (Atom)