Showing posts with label KUKU. Show all posts
Showing posts with label KUKU. Show all posts

Wednesday, August 23, 2017

UTUNZAJI WA KUKU NA MAGONJWA

Tunafahamu kwamba magonjwa ndio chanzo kikubwa cha kukatisha ndoto za mfugaji kutokana na ughali wa bei za dawa au vifo vinavyosababishwa na magonjwa hayo. Lakini upo uwezekano wa kuyaepuka hayo ikiwa tutazingatia yafuatayo kwa uangalifu mkubwa:-


  • Chanja kuku dhidi ya magonjwa mbalimbali yasiyotibika kama vile mdondo, gumboro na ndui.
  • Usifuge kuku na ndege wengine kama vile bata, kanga au kwale katika banda moja. Pia usichannganye kuku wa asili na wa kisasa katika banda moja, yaan kwa mfano usichanganye kuku wa nyama(broilers) na kuku wa asili.
  • Usirudishe nyumbani kuku waliopelekwa sokoni wakakosa soko kwani wanaweza kuleta magonjwa.
  • Ondoa kuku wote wenye dalili za ugonjwa na uwatibu kwa dawa husika, na waliokufa wazike au wachome moto.
  • Watenge kuku wageni kwa takribani wiki mbili kabla ya kuwachanganya na wa zamani.
  • Usafi wa banda, vyombo vya maji na kulishia, na muhudumu ni vya kuzingatia pia.
  • Zuia watu wasiohusika, au ndege kuingia au kukaribia banda.
  • Kuwepo mavazi na viatu maalum vya kuingilia bandani.
  • Mlangoni kuwekwe dawa ya kuulia vijidudu kwa ajili ya kukanyaga kabla ya kuingia bandani.
  • Banda lipumzishwe wiki mbili kabla ya kuingiza kuku wapya.
  • Wape kuku chakula bora na maji safi na salaama. Maji safi na salaama ni yale ambayo hata wewe mfugaji unaweza kuyanywa.




https://drive.google.com/file/d/0B_gpXEIUPoorUi1PTmdncXc5WDQ/view?usp=sharing
PATA KITABU HAPA

Thursday, August 11, 2016

MAGONJWA NA TIBA YAKE




habari za wakati huu wapendwa wafugaji na wasio wafugaji,wasomi wamachapisho yetu kwa ujumla.katika toleo hili tunachambua magonjwambalimbali ya kuku.magonjwa ya kuku husabibishwa na vitu mbali mbaliikiwemo virusi,minyoo,bakteria,uchafu,wadudu na hata upungufu wavirutubisho katika vyakula vya kuku hawa.magonjwa ambayo husababishwana virusi hua ni vigumu sana kutibika hivyo mfugaji hushauliwa kuwapachanjo ya magonjwa hayo.mfano ni mdondo(new castle disease).ugonjwahuu ni hatari sana kwa kua humaliza kuku wengi kwa wakati mmoja.wenginehuita huu ugonjwa kideri.
   Mdondo(new castle disease). 
kama binadamu aogopavyo ugonjwa wa UKIMWI,basi wafugaji wengihuogopa sana ugonjwa wa mdondo,pia huitwa kideli(newcastle disease).huuni ugonjwa HATARI unaosababishwa na virusi pia ni ugonjwa huu haunatiba.Hivyo mfugaji anatakiwa kuwapa chanjo mapema kabla ugonjwahaujafika eneo hilo.dalili za mdondo ni kama.
1.kuku kukohoa au kuhema kwa tabu 
2.manyoya ya kuku huvurugika na kua katika hali isiyo ya kawaida.
3.kuku huarisha kinyesi cha kijani
3.kupoteza hamu ya kula na mabawa kupoza
4.kizunguzungu na kuanguka chali
5.kupoteza fahamu 

ugonjwa huu hupelekea kuku wengi kufa kufikia hadi asilimia 50 hadi 100 kama usipo dhibitiwa mapema.
Namna ya ugonjwa unavyosambaa
1.virusi hawa huweza kusambaa kwa njia ya hewa au upepo husafirishavirusi hawa.
2.kinyesi cha kuku mwenye mdondo kikikanyagwa na mtu,baiskeli auwanyama wengine na kusafirishwa kwenye banda la kuku,ugonjwa huuhuweza pia kusambaa.
3.kuku alie kufa kwa mdondo asipo zikwa vizuri au kuchomwa moto,kukumzima akila mabaki hayo,kuku hao watakua katika hatari ya kupata mdondo.
JINSI YA KUPAMBANA NA MDONDO
Kama ilivyo elezwa hapo juu,gonjwa hili halina tiba.lakini kuku wakipewachanjo kwa wakati hua katika usalama.kuna chanjo kama;
1.LASOTA
chanjo hii ni ya vidonge,kidonge kimoja huchanganjwa na maji safi.chanjo hiitolewa baada ya siku tatu kisha rudi baada ya wiki tatu  na rudia kila baadaya majuma manne au kutokana na uonavyo.kabla ya kuku kupewa dawa hiiyapaswa wasipewe maji kwa masaa kadhaa kwa siku hio na muda wa kupewa maji basi wapewe sehemu yenye kivuli.
chanjo hii hupatikana katika maduka mbali mbali ya mifugo.
2.Chanjo ya Thermostable 1-2,dawa hii inahuwezo mkubwa wa kustahimili joto,watu wasio na majokofu basi tumia dawa hii ila hifadhi sehem kavu na isio na joto.dawa  hii huweza kukaa wiki mbili baada ya kufunguliwa kwa Mara ya kwanza.
EPUKA YAFUATAYO
kununua kuku katika minada na kuleta bandani 
kuruhusu kila mtu kuingia katika banda la kuku
kuacha mabaki ya kuku walikufa ovyo katika mazingira ya kuku
pia,endapo kuku wengi walikufa katika banda hilo basi ni vyema usilete kuku wengine katika banda hilo angalau kwa ,mwezi au zaid.
Tenganisha kuku wenye dalili za ugonjwa na kuku wengine.
ZINGATIA USAFI WA BANDA NA VYOMBO VYA KUKU WAKO.

usikose kutembelea blog hii kwa taarifa nyingine zaidi kuhusu ufugaji wa kuku

MASHINE YA KUANGULIA MAYAI YA KUKU



Habari za wakati huu wafuatiliaje wa machapisho yetu.Leo tutatazamia njia kuu mbili za kutotoresha mayai ya kuku wa kienyeji,njia hizo ni kumuacha kuku kutotoa mwenyewe na kumuwekea mazingira.njia ya pili ni kwa kutumia mashine za kutotoreshea.


NJIA ASILIA
kwa kutumia njia hii kuku ataachwa kutaga,kuatamia,na kutotoa mwenywe.mfugaji aandae mabox au mfuko kisha aweke vitu vyenye kutunza joto kama mchanga au matambaa kisha mabox hayo yawekwe katika mabanda ya kuku sehemu tulivu na yenywe kivuli


kuku hugata mayai 10-14 kutegemeana na aina ya kuku.kuku huweza kutotoa mayai 8-14


NJIA YA KISASA
Baada ya kuandaa sehemu ya kuku kutagia,kusanya mayai kila siku na kuweka katika trei.Uwekaji wa mayai hayo,sehemu kubwa ya yai iwe juu na incha yake iangalie chini.Hii husaidia katika utotoleshaji kwenye mashine.mashine hutotoresha vizuri zaidi endapo mayai yatakua yalikusanywa katika kipindi kifupi kuanzia siku 1-6 na kuwekwa katika mashine (incubator)

 MASHINE YA KUTOTORESHEA VIFARANGA(INCUBATOR)
Hii ni mashine ambayo hufanya kazi ya kuatamia na kutotoa mayai.mashine ina uwezo wa kutoto mayai mengi,mashine ndogo huweza kutotoa mayai 25-50.mashine hii hutoa joto sawa na joto la tetea,inashauliwa kugeuza geuza mayai kwa siku angalau mara tatu katika mashine ili kupata mazao bora zaidi.










CHANGAMOTO YA MASHINE HII
Inahitaji utaalamu kuitumia
inahitaji muda mwingi kukaa nayo karibu
ni gharama kuiendesha.





AINA / KOO ZA KUKU




Kuna Koo nyingi za kuku wa asili zinazopatikana hapa nchini.

                                   KOO

Baadhi ya Koo hizo na sifa zake ni hizi zifuatazo:



                               1.   Kuchi: 



                            Sifa zake za Kuchi:

a)      Ana umbo lenye ukubwa wa wastani.
b)      Hana upanga kichwani.
c)      Ana mdomo mfupi.
d)     Ana shingo ndefu yenye manyoya.
e)      Ana ngozi ya rangi ya njano
f)       Ana miguu mirefu isiyo na manyoya
g)      Ana uwezo mkubwa wa kujihami
h)      Wanapatikana mikoa ya Tabora, Singida, Shinyanga, Mwanza, na Tanga.



2 Kishingo:

              Sifa zake za Kishingo:

Ø  Ana umbo lenye ukubwa wa wastani 
Ø  Ana upanga kichwani.
Ø  Ana shingo isiyo na manyoya.
Ø  Ana ngozi yenye rangi ya njano au nyeusi.
Ø  Ana miguu mifupi isiyo na manyoya.
Ø  Anapatikana mikoa yote ya Tanzania. 

                        3 Bukini:
        Sifa zake za Bukini :

Ø  Ana umbo fupi na ni mnene.
Ø  Ana upanga kichwani.
Ø  Ana shingo yenye manyoya.
Ø  Ana ngozi yenye rangi ya njano.
Ø  Hana manyoya ya mkia.
Ø  Wanapatikana kwa wingi katika mikoa ya Tanga, Pwani, Kilimanjaro, na Singida.
                                 Ana miguu mifupi isiyo na manyoya.
           o   Ana miguu mifupi isiyo na manyoya.



     4  Kinyavu / nungunungu/kuchere:

            Sifa zake Kinyavu:

Ø  Ana umbo dogo akilinganishwa na Kishingo na Kuchi
Ø  Ana shingo yenye manyoya.
Ø  Ana ngozi yenye rangi ya njano.
Ø  Ana manyoya yaliyosimama.
Ø  Ana mkia mrefu wa wastani.
Ø  Anapatikana katika mikoa yote nchini.
        5  Kawaida /Kitewe:

            Sifa zake Kawaida / Kitewe:

Ø  Ana umbo dogo ukilinganisha na Kuchi au Kishingo.
Ø  Ana shingo yenye manyoya.
Ø  Ana ngozi yenye rangi nyeupe, njano au nyeusi
Ø   Ana manyoya ya mkia yenye urefu wa wastani.
Ø  Anapatikana mikoa yote ya Tanzania.

HISTORIA YA KUKU TANGIA KUUMBWA KWA DUNIA-KIBARA

HISTORIA YA KUKU (WAMETOKA WAPI?)

Kuku alitokana na jamii ya kuku-mwitu mwekundu wa Asia. Muda si muda, mwanadamu alitambua kwamba kuku anaweza kufugwa kwa urahisi. Inashangaza kwamba miaka 2,000 hivi iliyopita, Yesu Kristo alizungumzia jinsi kuku anavyokusanya vifaranga vyake na kuvilinda chini ya mabawa yake. (Mathayo 23:37; 26:34) Mfano huo unaonyesha kwamba kwa ujumla watu walimfahamu sana ndege huyo. Lakini kuku walianza kufugwa kwa wingi na mayai kutagwa kwa minajili ya biashara katika karne ya 19.
Leo nyama ya kuku inapendwa sana kuliko nyama ya ndege mwingine yeyote. Kuku hufugwa na mamilioni ya watu—hata wale wanaoishi mijini—kwa ajili ya chakula na biashara. Kwa kweli, ni wanyama wachache sana wa kufugwa wanaoweza kusitawi katika maeneo mbalimbali kama kuku. Nchi mbalimbali zimekuza kuku wa jamii fulani ambao wanaweza kukidhi mahitaji yao na kustahimili hali ya hewa ya sehemu hizo. Baadhi ya jamii hizo ni: kuku wa Australorp kutoka Australia; kuku ajulikanaye sana wa Leghorn, asili yake ni Mediterania lakini anapendwa sana nchini Marekani; kuku wa New Hampshire, kuku wa Plymouth Rock, kuku wa Rhode Island Red,na Wyandotte, kuku hao wanatoka Marekani; na Cornish, Orpington, na Sussex, wanatoka Uingereza.

Sayansi ya kisasa imefanya ufugaji wa kuku uwe mojawapo ya utendaji wenye faida sana katika kilimo. Nchini Marekani, wakulima hutumia mbinu bora za ulishaji na ufugaji. Wao pia hudhibiti magonjwa ya kuku kwa njia za kisayansi. Watu wengi hushutumu mbinu hizo za kisayansi za kuzalisha kuku wengi kuwa za ukatili. Lakini licha ya shutuma hiyo wakulima wangali wanabuni njia bora zaidi za kufuga ndege hao. Hivi sasa mtu mmoja tu anaweza kutunza kuku 25,000 hadi 50,000 akitumia mbinu za kisasa. Ndege hao huwa wamefikia uzani wa kutosha kuuzwa sokoni baada ya miezi mitatu tu.*

Chanzo cha Nyama

Waweza kuona nyama ya kuku ikiuzwa karibu kila mahali, iwe hotelini, mkahawani, au kwenye soko la nyama na vinywaji. Kwa kweli, mikahawa mingi ulimwenguni pote huuza hasa kuku. Jamii fulani hupika nyama ya kuku kunapokuwa na sherehe za pekee. Na katika baadhi ya nchi, kama vile India, mapishi mbalimbali ya kuvutia ya kuku yamebuniwa. Mapishi kama vile lal murgi,kuku aliyepikwa kwa pilipili-hoho; kurgi murgi, kuku aliyechanwa; na adrak murgi, kuku aliyepikwa kwa mchuzi wa tangawizi, huwa na ladha sana!

Mbona kuku wanapendwa sana? Kwanza, ni vyakula vichache tu vinavyoweza kutayarishwa kwa kutumia vikolezo mbalimbali. Wewe hupenda kuku aliyepikwaje? Je, unapenda kuku aliyekaangwa, aliyechomwa, aliyebanikwa, aliyepikwa kwa mvuke, au aliyechemshwa polepole? Ukitazama kitabu chochote cha mapishi huenda ukaona mapishi mengi sana ya kuku yanayokusudiwa kuboresha ladha ya kuku.
Kuku huuzwa kwa bei nafuu pia kwa sababu wanapatikana katika nchi nyingi. Wataalamu wa lishe hupendekeza nyama ya kuku, kwa sababu ina protini, vitamini, na madini ambayo ni muhimu kwa afya. Na bado, nyama ya kuku ina kalori chache, asidi-mafuta chache, na mafuta mengine.

Kulisha Nchi Zinazositawi

Bila shaka, nchi nyingine hazina bidhaa tele za kuku. Jambo hilo lapasa kufikiriwa kwa sababu ripoti ya tume maalumu ya Baraza la Sayansi ya Kilimo na Tekinolojia, ilisema hivi: “Idadi ya watu ulimwenguni inatarajiwa kuongezeka kufikia bilioni 7.7 mwaka wa 2020 . . . Hata hivyo, sehemu kubwa (asilimia 95) ya ongezeko hilo inatarajiwa kutukia katika nchi zinazositawi.” Taarifa hiyo inatisha zaidi unapofikiria kwamba tayari watu wapatao milioni 800 wana utapiamlo!

Hata hivyo, wataalamu wengi wanaona kwamba kuku wanaweza kutumiwa kulisha watu hao wenye njaa na wakulima wanaweza kupata riziki kwa kuuza kuku. Tatizo ni kwamba si rahisi kwa wakulima maskini kufuga kuku wengi sana. Jambo la kwanza ni kwamba katika nchi maskini kuku hufugwa hasa kwenye mashamba madogo vijijini, au katika vizimba vidogo. Na katika nchi hizo, kwa kawaida kuku hawatunzwi katika mazingira salama. Wakati wa mchana kuku huachiliwa ili wazurure-zurure ovyo na kutafuta chakula, kisha hurejea nyumbani usiku, nyakati nyingine wanalala mitini au katika vizimba vya mabati.

Si ajabu kwamba kuku wengi wanaotunzwa hivyo hufa—baadhi yao kutokana na ugonjwa hatari wa Newcastle na wengine huuawa na wanyama na wanadamu. Wakulima wengi hawana ujuzi wala uwezo wa kulisha kuku wao ifaavyo, hawawezi kuwatengenezea makao yafaayo, au kuwalinda na magonjwa. Ndiyo sababu miradi ya kuwaelimisha wakulima katika nchi zinazositawi imeanzishwa. Kwa mfano, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, hivi majuzi lilianzisha mradi wa miaka mitano wa “kuwasaidia wakazi maskini wa Afrika wanaoishi mashambani kupitia ufugaji wa kuku.”


Tungali twasubiri kuona matokeo ya jitihada hizo nzuri. Basi ni jambo lifaalo kwa wakazi wa nchi tajiri kutambua kwamba mlo wanaoona kuwa wa kawaida kwao kama vile kipande cha kuku yamkini ni mlo ghali sana kwa watu wengi duniani. Kwa watu hao, kula kuku ni kama ndoto tu.


                                                          WASILIANA NASI KWA; 


             

                                                                        0767-574 013
                                                              karolialex076@gmail.com