Tunafahamu kwamba magonjwa ndio chanzo kikubwa cha kukatisha
ndoto za mfugaji kutokana na ughali wa bei za dawa au vifo vinavyosababishwa na
magonjwa hayo. Lakini upo uwezekano wa kuyaepuka hayo ikiwa tutazingatia
yafuatayo kwa uangalifu mkubwa:-
- Chanja kuku dhidi ya magonjwa mbalimbali yasiyotibika
kama vile mdondo, gumboro na ndui.
- Usifuge kuku na ndege wengine kama vile bata, kanga au
kwale katika banda moja. Pia usichannganye kuku wa asili na wa kisasa
katika banda moja, yaan kwa mfano usichanganye kuku wa nyama(broilers) na
kuku wa asili.
- Usirudishe nyumbani kuku waliopelekwa sokoni wakakosa
soko kwani wanaweza kuleta magonjwa.
- Ondoa kuku wote wenye dalili za ugonjwa na uwatibu kwa
dawa husika, na waliokufa wazike au wachome moto.
- Watenge kuku wageni kwa takribani wiki mbili kabla ya
kuwachanganya na wa zamani.
- Usafi wa banda, vyombo vya maji na kulishia, na
muhudumu ni vya kuzingatia pia.
- Zuia watu wasiohusika, au ndege kuingia au kukaribia
banda.
- Kuwepo mavazi na viatu maalum vya kuingilia bandani.
- Mlangoni kuwekwe dawa ya kuulia vijidudu kwa ajili ya
kukanyaga kabla ya kuingia bandani.
- Banda lipumzishwe wiki mbili kabla ya kuingiza kuku
wapya.
- Wape kuku chakula bora na maji safi na salaama. Maji
safi na salaama ni yale ambayo hata wewe mfugaji unaweza kuyanywa.
PATA KITABU HAPA |
No comments:
Post a Comment