Wednesday, November 16, 2016

JINSI KIFARANGA KINAVYO TOTOLEWA KUTOKA SIKU 1-21 KUTOKA

TAFADHALI REJEA HII


JIFUNZE HII

                                                                  

UANDAAJI WA CHAKULA CHA KUKU

RLDC na Uboreshaji wa Maisha Vijijini Shirika la Rural Livelihood Development Company (RLDC ni moja ya mafanikio ya ushirikaiano kati ya Tanzania na Uswisi kwenye mchakato wa kupambana na umaskini na kuboresha maisha ya jamii za vijijini. Hii ni taasisi isiyo ya kibiashara ili yoanzishwa mwaka 2005 na mashirika ya Intercooperation na Swisscontact, lengo kuu likiwa kutekeleza Programu ya kuendeleza maisha ya jamii za vijijini (RLDP). Programu hii inasha bihiana na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupambana na Umaskini (MKUKUTA). Dhamira kuu ya RLDC ni Kuendeleza/kuboresha mifu mo ya masoko ili kuwawezesha wazalishaji wa vijijini kutumia fursa zilipo kuboresha maisha yao. Kwa sasa, RLDC inatelekeleza awamu ya pili ya mpango wake (2008-2011) na inaweka msukumo zaidi kwenye uendelezaji wa mifumo ya masoko. RLDC inafanya kazi katika mikoa sita ya Kanda ya kati-Dodoma, Singida, Morogoro, Shinyanga, Tabora, na Manyara. Jamii nyingi maskini zinaishi katika ukanda huu wenye sehemu kubwa yenye hali ya mvua chache na nusu jangwa inayostawisha shughuli chache za kiuchumi. Hata hivyo kuna fursa nyingi sana zinazoweza kutoa ajira na kuboresha ya jamii zake. RLDC inafadhiliwa na Serikali ya Uswisi kupitia shirika la Uswisi la maendeleo (SDC). Kwa sasa RLDC inawezesha sekta za pamba, alizeti, maziwa, ufugaji wa kuku wa kienyeji, mpunga na habari kupitia vipindi vya redio kwa ajili ya wazalishaji wa vijijini. “RLDC inaboresha mifumo ya masoko ili kuwezesha wazalishaji wa vijijini kuinua maisha yao”




Thursday, August 11, 2016

MAGONJWA NA TIBA YAKE




habari za wakati huu wapendwa wafugaji na wasio wafugaji,wasomi wamachapisho yetu kwa ujumla.katika toleo hili tunachambua magonjwambalimbali ya kuku.magonjwa ya kuku husabibishwa na vitu mbali mbaliikiwemo virusi,minyoo,bakteria,uchafu,wadudu na hata upungufu wavirutubisho katika vyakula vya kuku hawa.magonjwa ambayo husababishwana virusi hua ni vigumu sana kutibika hivyo mfugaji hushauliwa kuwapachanjo ya magonjwa hayo.mfano ni mdondo(new castle disease).ugonjwahuu ni hatari sana kwa kua humaliza kuku wengi kwa wakati mmoja.wenginehuita huu ugonjwa kideri.
   Mdondo(new castle disease). 
kama binadamu aogopavyo ugonjwa wa UKIMWI,basi wafugaji wengihuogopa sana ugonjwa wa mdondo,pia huitwa kideli(newcastle disease).huuni ugonjwa HATARI unaosababishwa na virusi pia ni ugonjwa huu haunatiba.Hivyo mfugaji anatakiwa kuwapa chanjo mapema kabla ugonjwahaujafika eneo hilo.dalili za mdondo ni kama.
1.kuku kukohoa au kuhema kwa tabu 
2.manyoya ya kuku huvurugika na kua katika hali isiyo ya kawaida.
3.kuku huarisha kinyesi cha kijani
3.kupoteza hamu ya kula na mabawa kupoza
4.kizunguzungu na kuanguka chali
5.kupoteza fahamu 

ugonjwa huu hupelekea kuku wengi kufa kufikia hadi asilimia 50 hadi 100 kama usipo dhibitiwa mapema.
Namna ya ugonjwa unavyosambaa
1.virusi hawa huweza kusambaa kwa njia ya hewa au upepo husafirishavirusi hawa.
2.kinyesi cha kuku mwenye mdondo kikikanyagwa na mtu,baiskeli auwanyama wengine na kusafirishwa kwenye banda la kuku,ugonjwa huuhuweza pia kusambaa.
3.kuku alie kufa kwa mdondo asipo zikwa vizuri au kuchomwa moto,kukumzima akila mabaki hayo,kuku hao watakua katika hatari ya kupata mdondo.
JINSI YA KUPAMBANA NA MDONDO
Kama ilivyo elezwa hapo juu,gonjwa hili halina tiba.lakini kuku wakipewachanjo kwa wakati hua katika usalama.kuna chanjo kama;
1.LASOTA
chanjo hii ni ya vidonge,kidonge kimoja huchanganjwa na maji safi.chanjo hiitolewa baada ya siku tatu kisha rudi baada ya wiki tatu  na rudia kila baadaya majuma manne au kutokana na uonavyo.kabla ya kuku kupewa dawa hiiyapaswa wasipewe maji kwa masaa kadhaa kwa siku hio na muda wa kupewa maji basi wapewe sehemu yenye kivuli.
chanjo hii hupatikana katika maduka mbali mbali ya mifugo.
2.Chanjo ya Thermostable 1-2,dawa hii inahuwezo mkubwa wa kustahimili joto,watu wasio na majokofu basi tumia dawa hii ila hifadhi sehem kavu na isio na joto.dawa  hii huweza kukaa wiki mbili baada ya kufunguliwa kwa Mara ya kwanza.
EPUKA YAFUATAYO
kununua kuku katika minada na kuleta bandani 
kuruhusu kila mtu kuingia katika banda la kuku
kuacha mabaki ya kuku walikufa ovyo katika mazingira ya kuku
pia,endapo kuku wengi walikufa katika banda hilo basi ni vyema usilete kuku wengine katika banda hilo angalau kwa ,mwezi au zaid.
Tenganisha kuku wenye dalili za ugonjwa na kuku wengine.
ZINGATIA USAFI WA BANDA NA VYOMBO VYA KUKU WAKO.

usikose kutembelea blog hii kwa taarifa nyingine zaidi kuhusu ufugaji wa kuku

MASHINE YA KUANGULIA MAYAI YA KUKU



Habari za wakati huu wafuatiliaje wa machapisho yetu.Leo tutatazamia njia kuu mbili za kutotoresha mayai ya kuku wa kienyeji,njia hizo ni kumuacha kuku kutotoa mwenyewe na kumuwekea mazingira.njia ya pili ni kwa kutumia mashine za kutotoreshea.


NJIA ASILIA
kwa kutumia njia hii kuku ataachwa kutaga,kuatamia,na kutotoa mwenywe.mfugaji aandae mabox au mfuko kisha aweke vitu vyenye kutunza joto kama mchanga au matambaa kisha mabox hayo yawekwe katika mabanda ya kuku sehemu tulivu na yenywe kivuli


kuku hugata mayai 10-14 kutegemeana na aina ya kuku.kuku huweza kutotoa mayai 8-14


NJIA YA KISASA
Baada ya kuandaa sehemu ya kuku kutagia,kusanya mayai kila siku na kuweka katika trei.Uwekaji wa mayai hayo,sehemu kubwa ya yai iwe juu na incha yake iangalie chini.Hii husaidia katika utotoleshaji kwenye mashine.mashine hutotoresha vizuri zaidi endapo mayai yatakua yalikusanywa katika kipindi kifupi kuanzia siku 1-6 na kuwekwa katika mashine (incubator)

 MASHINE YA KUTOTORESHEA VIFARANGA(INCUBATOR)
Hii ni mashine ambayo hufanya kazi ya kuatamia na kutotoa mayai.mashine ina uwezo wa kutoto mayai mengi,mashine ndogo huweza kutotoa mayai 25-50.mashine hii hutoa joto sawa na joto la tetea,inashauliwa kugeuza geuza mayai kwa siku angalau mara tatu katika mashine ili kupata mazao bora zaidi.










CHANGAMOTO YA MASHINE HII
Inahitaji utaalamu kuitumia
inahitaji muda mwingi kukaa nayo karibu
ni gharama kuiendesha.





AINA / KOO ZA KUKU




Kuna Koo nyingi za kuku wa asili zinazopatikana hapa nchini.

                                   KOO

Baadhi ya Koo hizo na sifa zake ni hizi zifuatazo:



                               1.   Kuchi: 



                            Sifa zake za Kuchi:

a)      Ana umbo lenye ukubwa wa wastani.
b)      Hana upanga kichwani.
c)      Ana mdomo mfupi.
d)     Ana shingo ndefu yenye manyoya.
e)      Ana ngozi ya rangi ya njano
f)       Ana miguu mirefu isiyo na manyoya
g)      Ana uwezo mkubwa wa kujihami
h)      Wanapatikana mikoa ya Tabora, Singida, Shinyanga, Mwanza, na Tanga.



2 Kishingo:

              Sifa zake za Kishingo:

Ø  Ana umbo lenye ukubwa wa wastani 
Ø  Ana upanga kichwani.
Ø  Ana shingo isiyo na manyoya.
Ø  Ana ngozi yenye rangi ya njano au nyeusi.
Ø  Ana miguu mifupi isiyo na manyoya.
Ø  Anapatikana mikoa yote ya Tanzania. 

                        3 Bukini:
        Sifa zake za Bukini :

Ø  Ana umbo fupi na ni mnene.
Ø  Ana upanga kichwani.
Ø  Ana shingo yenye manyoya.
Ø  Ana ngozi yenye rangi ya njano.
Ø  Hana manyoya ya mkia.
Ø  Wanapatikana kwa wingi katika mikoa ya Tanga, Pwani, Kilimanjaro, na Singida.
                                 Ana miguu mifupi isiyo na manyoya.
           o   Ana miguu mifupi isiyo na manyoya.



     4  Kinyavu / nungunungu/kuchere:

            Sifa zake Kinyavu:

Ø  Ana umbo dogo akilinganishwa na Kishingo na Kuchi
Ø  Ana shingo yenye manyoya.
Ø  Ana ngozi yenye rangi ya njano.
Ø  Ana manyoya yaliyosimama.
Ø  Ana mkia mrefu wa wastani.
Ø  Anapatikana katika mikoa yote nchini.
        5  Kawaida /Kitewe:

            Sifa zake Kawaida / Kitewe:

Ø  Ana umbo dogo ukilinganisha na Kuchi au Kishingo.
Ø  Ana shingo yenye manyoya.
Ø  Ana ngozi yenye rangi nyeupe, njano au nyeusi
Ø   Ana manyoya ya mkia yenye urefu wa wastani.
Ø  Anapatikana mikoa yote ya Tanzania.

WASIFU NA MAWASILIANO

JINA:   KAROLI ALEX

SIMU NAMBA:  0767 574 013

E-MAIL-  karolialex076@gmail.com

LOCATION OF PROJECT:  Namibu,Kibara,Bunda,Mara,Tanzania



UENDESHAJI WA MRADI WA KUKU-KIBARA

 UENDESHAJI WA MRADI WA KUKU WA MAYAI:

Iili kufanikiwa kufikia malengo ya kufuga kuku wa mayai  ni vyema mfugaji akapata wasaa wa kujiuliza maswali kadhaa ili awe na dira sahihi ya kile anachotarajia kufanya kutokana na mapato ya mradi huo.
Dira ni picha ya matokeo yanayotarajiwa yanayotokana na juhudi na maarifa .
Bila shaka kabla ya kuanza kufuga utakuwa umejiuliza ni kwa nini ufuge kuku wa mayai na wala sio kufanya kitu kingine ; swali kama hili litakusaidia kuwa na muelekeo wa kile unachotarajia na hivyo kuweka mkakati sahihi wa kusimamia mradi wako wa kuku wa mayai.Mfano , pengine umeamua kufuga kuku kwasababu kuna upatikanaji wa pembejeo kwa urahisi kama vile upatikanaji wa vifaranga, viinilishe, madawa na kubwa zaidi ni upatikanaji wa soko la mazao yako.
Vyovyote iwavyo mambo yafuatayo ni vizuri yakazingatiwa ili kupata mafanikio katika mradi wa kufuga kuku wa mayai;
1.      Uwe na uhakika wa kupata vifaranga kutoka kwa wasambazaji mahiri     ( reliable Day old Chicks breeders and Suppliers)
2.      Zingatia ratiba ya kulisha. Lisha kuku  chakula kinachopendekezwa kwa kuzingatia umri  na uzito.
3.      kagua na na fanya usafi mara kwa mara na katika nyakati zilizopangwa(inspect and carry out specificl and periodical hygienic operations)
4.      toa matunzo kwa kwa kuzingatia mahitaji ya makundi.
 
5.      Tengeza viota ili kuku waweze kutaga mayai kwa faragha bila bughudha kutoka kwa wengine. Vilevile viota husaidia kuwa na mayai safi na husaidia kuepuka kuvunja kuvunjika na kuchafuka kwa mayai mara kwa mara.
6.      Hakikisha unasafisha mayai kwa kitambaa safi  baada ya kuokota na kabla kuwauzia wateja.
7.      Zingatia matakwa ya wateja kwa kuainisha mayai katika makundi kama ifuatavyo;
  • Rangi ya mayai
  • Rangi ya kiini cha yai(egg yolk colour), wengi wanapenda kiini cha rangi ya njano.
  • Ukubwa wa mayai
  • Aina ya mayai( mayai ya kienyeji yanapendwa zaidi kuliko ya kisasa)
8.      Fanya ukaguzi wa afya za kuku na kuwa tibu kila mara. Utaratibu unaopendekezwa ni kukagua afya asubuhi unapoamka na usiku unapoenda kulala. Angalia vinyeo ili kuona wanakunya kinyesi cha rangi gani(kinyesi ni kielelezo muhimu katika kutambua ugonjwa).
9.      Chunguza tabia za kuku ili kuona kama wanakula mayai au la . Ukiona kuku wameanza kula mayai fanya zoezi la kukata midomo mara moja kazi hufanywa na wataalamu , kwahiyo unashauriwa kumuona mtaalmu aliye jirani.
10.  Tunza kumbukumbu zote mradi  ili zikusaidie kufanya tathmini ya mradi unaoendesha.